Chimbuko mtifuano kati ya Urusi na Ukraine
Mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, ni wa muda mrefu, haujaanza mwaka mmoja au miwili iliyopita, bali ina takriban miaka 10 nyuma.
Novemba 21, 2013, Rais wa Ukraine, Victor Yanukovich inadaiwa aliahirisha kutia saini makubaliano baina ya Ukraine na Umoia wa Ulaya kuanzisha ushirika na ilikuwa ni sababu ya maandamano ya hadhara yaliyoungwa mkono na nchi za Ulaya na baadaye yaliyopata kuwa mapambano ya kivita ya muda mrefu.
Huu ndio mwanzo wa mgogoro wa kisiasa unaoendelea hadi leo na kuachishwa kazi kwa Rais Yanukovich.
Mei 2, 2014, wafuasi wa vikundi vya utaifa na siasa kali nchini Ukraine vilidaiwa kuwazuia watu waliopinga maandamano ya "Euromaidan" katika jumba la vyama vya wafanyakazi mjini Odessa wasitoke nje na kuchoma moto jumba hilo, watu 48 wakiwemo wanawake saba na mtoto mmoja walidaiwa kufariki huku wengine 200 wakijeruhiwa.
Hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa na mamlaka wala mtu aliyeadhibiwa kwa kosa hilo la mauaj ya kiraia na hata matokeo ya upelelezi wa kesi ya mabingwa wa kupiga shabaha ya Euromaidan waliowapiga watu risasi wakati wa maandamano.
Matokeo ya kupinduliwa kwa serikali mwaka 2014 nchi ya Ukraine ilianza kujengwa kwenye misingi ya kinazi iliyomaanisha kukanusha mambo yote yanayohusika na Warusi ikiwa ni pamoja na utamaduni, desturi na tabia ya kipekee ya wenyeji wa maeneo makubwa ya kusini na mashariki mwa nchi ya Ukraine.
Haki na maslahi ya wenyeji wa sehemu za kusini na mashariki za Ukraine zimedharauliwa na kuharibiwa kwa nguvu za kijeshi huku serikali ya nchi ya Ukraine ikianza kuwatenda visivyo haki wenyeji wa Crimea, Donbass na maeneo ya kusini na mashariki na kuwachukulia wao kama wasio sehemu ya taifa hilo.
Awali, wenyeji wa Crimea waliokataa kuukubalia utawala na washirika wa uasi "Euromaidan" walifanya uchaguzi ili kujitoa kwenye eneo la Ukraine na baadaye vita katika Donbass imezuka, ambapo wenyeji waliitaka serikali ya Ukraine kuheshimu haki zao za kuongea lugha yao ya kiasili, kufanya masomo ya lugha hiyo kwa watoto wao pamoja na kuwakumbuka mashujaa wao waliookoa dunia dhidi ya wafashisti miaka 80 iliyopita.
Badala ya kuzingatia maoni yao, viongozi waliotawala mjini Kiev waliwashtaki wenyeji wa maeneo ya kusini-mashariki ya nchi kwa kuwaita ni wasaliti na magaidi huku wakipeleka jeshi na vikosi vya vikatili kuwakandamiza watu.
Hata hivyo, Ukraine imefanikiwa kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini umo. Nchi ya Urusi kama mpatanishi ilitoa mchango mkubwa. Februari 12, 2015, mkataba unaoitwa "Hatua kabambe za kutekeleza makubaliano ya Minsk" utiwe saini na kukubaliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mkataba huu wa "Hatua kabambe ikilenga kutekeleza makubaliano ya Minsk" na kutoa nafasi ya kufufua mipaka ya nchi ya Ukraine (bila ya Crimea). Lakini nafasi hiyo imeshindikana kutokana kile kinachoonekana wazi kuwa ni viongozi wa Kiev na nchi wadhamini wa Ulaya.
Nchi za Ujerumani na Ufaransa zinadaiwa kuupuuza utekelezaji wa vipengele vya mkataba huo huku waliokuwa viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Ukraine; Angela Merkel, Francois Hollande na Petr Poroshenko wakikiri kwamba hawakupanga kuufuata kwa manuiaa yao ya kuisafirishia silaha Ukraine.
Kutokana na hilo, muundo wa dola la Ukraine lililopata uhuru baada ya kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti umekuwa ukigawanyika kutoka ndani kwa muda mrefu.
Mipaka ya nchi hiyo haikutambuliwa na baadhi ya nchi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni msimamo wake mkali wa kutotekeleza masharti ya Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Madai ya Ukraine "Kuheshimu uzima wa mipaka" yake yamepoteza maana kwa sababu ya sera za nchi zinazoaminika kutumia rimoti kuiendesha serikali hiyo.
Serikali ya Vladimir Zelensky ilipoingia madarakani mwaka 2019, haikufanya mabadiliko yoyote chanya huku kiongozi huyo aliyeathiriwa na vikundi mbalimbali vya kisiasa vya ndani na nje akiendelea kuyapuuza makubaliano ya Minsk kwa kuongoza majadiliano ya kimataifa yasiyo na tija na kuchelewesha mchakato muhimu wa mazungumzo kati yake na Urusi bila sababu za msingi.
Kwa miaka mingi vikundi vya kijeshi vya Ukraine vilikuwa vikilipiga mizinga eneo la Donbass, huku vikiwakandamiza wenyeji wa eneo hilo kwa kuharibu uchumi na njia za usafrishaji, hivyo kusababisha wananchi wa eneo hayo kukubali itikadi kali ya kuchukiza Urusi zilifumbia macho unazi wa kisasa nchini humo.
Ukweli ni kwamba, sera ya Marekani na NATO ilikuwa ni kuibadilisha Ukraine kuwa adui wa Urusi.
Kwa muda wa zaidi ya miaka nane washauri wa kijeshi wa nchi wanachama wa NATO, walishiriki katika mchakato wa uundwaji wa majeshi ya Ukraine yenye uwezo wa kushambulia maeneo ya Donbass na Urusi.
Ndani ya mipaka ya Ukraine kulifanywa mafunzo ya kijeshi ya nchi za Magharibi, kulijengwa vituo vyao vya kijeshi na maabara za kibiolojia na kuliajiriwa vikosi vya Wanazi wanaoweza kutumiwa na NATO kwa ajili ya kutekeleza amri yoyote ile.
Serikali ya Ukraine na washirika wake wa nchi za magharibi zilitia mkazo mapambano dhidi ya utamaduni wa wenyeji wa nchi hiyo kwa kupagaza utamaduni wa Ukraine na kuangamiza utamaduni wa Warusi.
Ingawa lugha ya Kirusi ni ya uzawa kwa wananchi walio wengi wa Ukraine, serikali ya nchi hiyo imekataza utumiaji wa lugha hiyo katika jamii, imefunga shule za Urusi na imeweka vikwazo dhidi ya usambazaji wa vitabu, magazeti, filamu na nyimbo kwa lugha ya Urusi.
Urusi haikuweza kuifumbia macho sera ya miaka minane ya serikali ya Ukraine.
Mwishoni mwa mwaka 2021 Urusi iliandaa na kupeleka kwa nchi za magharibi mapendekezo yake ya kuhakikisha dhamana za kisheria za usalama. Dhamana hizo zilimaanisha kaasharikitak una ya ia kureaty metindo wa kijeshi wa jumuiya hiyo katika hali ya mwaka 1997 wakati wa kusainiwa kwa mkataba mkuu kati ya Urusi na NATO.
Hata hivyo, mapendekezo hayo ya Urusi yalifutwa na nchi wanachama wa NATO. Hivyo Urusi haikuwa na njia nyingine zaidi ya kuutambua uhuru wa kujitawala wa Jamhuri za Watu ya Donetsk na Lugansk na Februari 21, 2022, na baadaye Septemba 30, 2023 kuzikubali Jamhuri hizo ziwe sehemu yake kutii dhamira za wenyeji waliopiga kura ya maoni ya kujiunga na Urusi.
Februari 24, 2022, Urusi ilipaswa kuanza operesheni maalum ya kijeshi ili kulilinda eneo la Donbass, kuzidhoofisha nafasi za kijeshi za Ukraine kuyashambulia maeneo ya Donbass na kuvizuia vikosi vya kinazi visiendelee nchini Ukraine na pia kujihami dhidi ya matishio na hatari kwa usalama wa Urusi kutoka Ukraine. Huu ndio mwanzo wa kile kinachoelezwa kuwa ni uvamizi wa Urusi.
Pamoja na hayo nchi za magharibi zinaendelea kuipa Ukraine silaha nyingi, kuwapa makamanda wa kijeshi wa Ukraine habari za upelelezi za aina mbalimbali na kushiriki katika uwekaji wa mipango na utekelezaji wa operesheni za kijeshi dhidi ya Urusi.
Nchi wanachama wa NATO wameingia kwenye vita kwa kujificha na kutumia vikosi vya kibinafsi vya kijeshi na watoaji wa maagizo.
Hivi karibuni nchi za magharibi zimezidisha kwa kiwango cha juu usafirishaji wa silaha za kufanya mashambulizi nchini Ukraine. Hatua hiyo inaifanya Ukraine iongeze ukali wa mzozo wa kivita na iendeshe vita kamili.
Ukraine inakiri kwamba ili kuishinda Urusi inahitaji silaha nzito za kisasa za kufanya mashambulizi. Inamaanisha kwamba nchi ya Ukraine ikisaidiwa na nchi za magharibi haiendeshi operesheni ya kujilinda bali ina dhamira za kuyashambulia maeneo.
Tangu mwanzo wa mzozo wa kivita katika Donbass mwaka 2014 wanajeshi wa Ukraine wanazishambulia kwa makusudi miundombinu muhimu ya kiraia hasa vituo vya kusambaza maji na nishati.
Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan anasema kuwa katika vita hiyo, Jeshi la Urusi linapoendesha operesheni maalum ya kijeshi linazishambulia miundombinu ya kijeshi za adui kwa kutumia silaha zinazoweza kulenga shabaha kwa usahihi na sio kuua watu.
Na mwandishi wa gazeti la Raia Mwema
Jumatano, Novemba 22-28, 2023