Посольство Российской Федерации в Объединенной Республике Танзании
+255-22-2666005
+255-22-2666006
/

Hiki hapa kinachohatarisha usalama wa chakula

Dunia ya leo imeingia zama ya mabadiliko makubwa ambayo yanaashiria mwisho wa utawala wa karne nyingi wa mataifa wakoloni - kwa maneno mengine, "matajiri bilioni moja" - waliozoea kuishi maisha ya neema kwa kuwanyonya wanyongwe.

Hata hivyo, hawakubali kupoteza ubabe wao, na kwa sababu hivo wanafanya kila juhudi kwa kuzidisha muda wao wenye utajiri na kukwamisha ujenzi wa dunia mpya yenye haki kwa wote pamoja.

Juhudi zao za kujihakikishia maisha yenye shibe wakati wengine wanadhurika kwa mlipuko wa UVIKO-19, zimesababisha changamoto za upatikanaji wa chakula ulimwenguni.

Hapo ndipo mataifa ya Magharibi yakaanza kuchapisha pesa bila sababu zozote za kiuchumi. Walichotaka kufanya ni kutatua changamoto zao zilizosababishwa na kudorora kwa uchumi.

Baada ya kuchapisha pesa (kiasi cha dola trilioni tisa katika Marekani na euro trilioni tano katika Ulaya), wakaanza kufyonza bidhaa za kilimo huku wakitumia vibaya ukiritimba wao wa kiuchumi na kuathiri nchi zinazoendelea.

Ukosefu wa usawa katika uchumi wa dunia, makosa ya ndani na kasoro katika sera za kiuchumi, nishati na chakula za mataifa ya Magharibi ni kati ya sababu zilizochangia mgogoro wa chakula duniani. Pia majanga ya tabia nchi na mlipuko wa UVIKO-19 viliyumbisha masoko ya dunia likiwemo soko la bidhaa za kilimo.

Bei za juu za mafuta zilizosababishwa pamoja na nia ya nchi za Magharibi kushinikiza utumiaji wa nishati mbadala, ziliongeza ushuru wa uchukuzi na bei za mbolea.

Halafu vita kati ya Urusi na Ukraine, kama, alivyokiri rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa ziarani nchini Cameroon mwezi Julai mwaka uliopita, imezorotesha mambo hasa katika sekta ya usalama wa chakula.

Ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba kilichozorotesha hali hivo ni vikwazo vingi dhidi ya Urusi. Athari zinaonekana waziwazi kwenye soko la chakula duniani,pia katika sekta za nishati na viwanda.

Baadhi ya nchi zilifunga magati ya bandari kwa bidhaa za kilimo na za viwanda za Urusi huku makapuni ya usafirishaji na taasisi za kifedha yakiwemo benki ya kimataifa yakikataa kutoa mikopo, kuweka bima na kufanya miamala kwa wafanyabiashara wa chakula na mbolea wa Kirusi.

Lakini nchi za Magharibi zilianza kuilaumu Urusi kwa kuzuka kwa mgogoro wa uhaba wa chakula huku zikificha ukweli kwamba wanaopata faida kubwa kutokana na kuongezeka kwa bei za chakula na kuvurugika kwa biashara na usafirishaji wa bidhaa za kilimo ni mashirika makubwa zaidi ya nchi za Magharibi.

Kuna kitu kinachoitwa "makubaliano ya nafaka" (au makubaliano ya Black Sea) juu ya usafirishaji wa chakula kutoka Ukraine kwa ajili ya nchi maskini zaidi.

Mwaka mmoja uliopita Urusi ilikubali kutia saini makubaliano hayo ingawa hakukuwa na nchi yoyote ilivojenga vizuizi vya usafirishaji wa nafaka kutoka bandari za Ukraine zilizopo Black Sea. Kilichojitokeza Ukraine yenyewe ilizuia bandari zake kwa kutega mabomu baharini hali iliyokwamisha mamia ya meli za kigeni kutia nanga.

Tofauti na Ukraine, jeshi la wanamaji la Urusi lilitangaza na kuhifadhi njia za usafirishaji wa bidhaa za kimsaada katika Black Sea. Urusi ikifahamu kuwa nchi zinazoendelea zikiwemo za Afrika zinazohitaji chakula hazipaswi kupata tabu, ilitesheleza mapendekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres kuhakikisha usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kwenda nchi maskini hautatizwi.

Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha hadi tarehe 15 Juni bidhaa za kilimo tani milioni 31.7 zimesafirishwa kutoka bandari za Ukraine. Bidhaa za kilimo tani elfu 976 kati ya tani milioni 31.7 sawa na asilimia 3.1 tu ndizo zimepelekwa Afrika (Djibouti, Somalia, Sudan, Libya na Ethiopia). Lakini bidhaa za kilimo tani milioni 12,3 sawa na asilimia 38.9 zimepelekwa katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Ingawa hali iko hivyo, nchi za Magharibi zinaendeleza propaganda kwamba Ukraine inaokoa dunia isife kwa njaa.

Ikumbukwe kwamba makubaliano ya Black Sea yalikuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni usafirishaji wa nafaka za Ukraine na ya pili kulingana na makubaliano hayo kama yalivyotajwa katika memoranda kati ya Urusi na UN yalilenga kuwezesha wauzaji wa Urusi wa chakula na mbolea kwenye soko la dunia watumie huduma za benki, mashirika ya bima na makampuni ya usafirishaji, na wanunue spea bila ya vikwazo.

Pia memoranda hiyo ina sharti la kurudisha usafirishaji wa ammonia kutoka Urusi hadi bandari ya Odessa, Ukraine ili kuiuza nje. Lakini Ukraine ilililipua bomba hilo la kusafirishia ammonia badala ya kutekeleza makubaliano hayo.

Kwa hiyo, sehemu ya makubaliano ya Black Sea yanayonufaisha Urusi hayatekelezwi kabisa. Si hivyo tu, nchi za Magharibi zimesema zinaendelea kuongeza vikwazo vya upandemmoja dhidi ya Urusi, bila ya kujali kuwa vikwazo hivyo vinaathiri usafirishaji wa chakula na mbolea kwenye soko la dunia zikiwemo nchi za Afrika.

Mbali ya hayo, nchi za Umoja wa Ulaya zinaendelea kushikilia, kinyume cha sheria, mizigo ya tani 300 000 za mbolea za Kirusi ambayo Rais Vladmir Putin aliagiza kuzipatia bure nchi maskini. Baada ya kufanya juhudi nyingi, Urusi iliweza kupeleka mbolea hizo katika nchi za Malawi (tani 20 000) na Kenya (tani 34 000). Urusi pia inaendesha mazungumzo ya kuupeleka mzigo wa mbolea (tani 34 000) nchi-ni Nigeria.

Ikumbukwe pia kwamba Urusi ipo tayari kuzipa nchi maskini kiasi hiki cha nafaka bila malipo yo yote. 

Na Mwandishi maalum wa

MwanaHalisi

Alhamisi, Julai 7, 2023