Посольство Российской Федерации в Объединенной Республике Танзании
+255-22-2666005
+255-22-2666006
/

Tanzania, Urusi zajivunia ushirikiano


NA MWANDISHI WA ZANZIBAR LEO

Serikali уа Mapinduzi Zanzibar imeleza kuwa itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirikisho la Urusi katika nyanja mbali mbali kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili.

Waziri wa nchi, ofisi va rais na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Jamal Kassim Ali alieleza hayo katika sherehe za miaka 62 va mahusiano baina ya nchi mbili hizo zilizofanyika katika hoteli ya maru maru, Mjini Unguja.

Jamal alieleza kuwa Teikota Mapinduzi ya Zanzibar inakaribisha kwa moyo wote wawekezaji kutoka urusi katika fani na sekta mbali mbali wakiwemo wa wasanii - wanamuziki na waigizaji ii kuimarisha uchumi wa Zanzibar na utamaduni wa mataifa hayo.

"Nimefurahi kuona kwamba kuna baadhi ya hatua zimechukuliwa katika mwelekeo ambao Kituo cha Utamaduni cha Tanzania na Urusi kimeendelea kupanuka na kuzindua miradi yake Zanzibar, hakika tunakaribisha kwa dhati mpango huu", alieleza Jamal.

Aliongeza kuwa kuzinduliwa kwa safari za ndege za moja kwa moja za kutoka jiji la Moscow hadi Zanzibar utatoa msukumo zaidi kwa uchumi wa kitaifa kwa kuongeza mtiririko wa watalii wanaoingia nchini.

Waziri Jamal pia alikumbushia zama za iliyokua Umoia wa Kisoviet wa nchi za Urusi (USSR) ambao ulikuwa na Ubalozi mdogo Zanzibar na kueleza kuwa ni shauku ya serikali kuona nchi hiyo inafungua tena ofisi zake tena siku za usoni.

Katika hatua nyengine Jamal alipongeza uamuzi wa kufunguliwa kwa madarasa ya lugha ya Kirusi Zanzibar akieleza kuwa utapanua maeneo va ushirikiano vakiwemo matukio ya kitamaduni yatakayopangwa ikiwemo matamasha, maonesho na matukio ya maendeleo ya elimu.

"Tunathamini nia niema inayoendelezwa na Urusi ambapoo katika mwaka huu, vyuo vikuu vya nchi hiyo vilishiriki kikamilifu katika uwasilishali wa fursa za elimu ambapo wanafunzi wa Zanzibar walialikwa kullunga navyo" aliongeza Jamal.

Awali akizungumza katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo Watanzania waliosoma, kufanya kazi na kuishi Urusi, Balozi wa Urusi nchini Tanzania Andrey Avetisyan alieleza kuwa nchi hiyo inajivunia uhusiano na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioasisiwa na wasisi wa mataifa hayo.

Alieleza kuwa nchi hiyo inajivunia uhusiano na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioasisiwa na wasisi wa mataifa hayo. Alieleza kuwa katika miaka yote hiyo, nchi mbili hizo zimeunganishwa na urafiki wa dhati, kuelewana na ushirikiano usioyumba katika nyanja ya kimataifa iambo linaloendelezwa na viongozi waliopo sasa.

Aidha alisema anaamini nchi mbili hizo zitaongeza kiwango cha uuhusiano na kuwa bora zaidi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni huku wakilenga kuumimarisha uhusiano huo i uwe na nguvu zaidi.

"Tunaposonga mbeletunatarajla kuendeleza mafanikio ya ushirikiano wa kibinadamu na pia katika uchumi. Ukweli kwamba mapokezi tunayoyapata hapa ni ushuhuda kwamba Urusi inathamini sana uhusiano huo, si tu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumba wake, bali pia kuwa na nia mahususu ya kuyaweka mizizi hapa Zanzibar” alieleza Balozi Andrey.

Zanzibar Leo

December 16, 2023, Saturday